Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ juzikati alizua kizaazaa kisa ujauzito
alipohudhuria kwenye msiba wa aliyekuwa bosi wa Tip Top Connection,
Abdul Taletale ‘Abdul Bonge’ aliyefariki dunia ghafla wikiendi
iliyopita.
Tukio hilo la Zari lilichukua nafasi katika Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Matombo mkoani hapa ambapo mastaa kibao walisafiri kutoka Dar kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo.
ILIKUWAJE?
Awali, katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa mapema Jumanne wiki hii, Zari na Diamond, wakiwa wameongozana na wapambe wao walifika eneo la msiba ambapo kwa taratibu za Kiislam, wanawake hawachanganyiki na wanaume hivyo Zari akachukuliwa kwenda upande mwingine huku Diamond akielekea upande wa wanaume.

HALI YA HEWA YABADILIKA
Mara baada ya mastaa hao kutinga eneo hilo, umati mkubwa uliokuwa msibani hapo ulianza kuwazingira huku kila mmoja akitaka kuwaona.
ZARI AIBUA KIZAAZAA
Akiwa upande wa wanawake wenzake, Zari alijikuta akizungukwa na baadhi ya watu walionekana wazi kumchunguza kuanzia miguuni hadi kichwani ikidaiwa kuwa, walikuwa wakicheki kama kweli ana mimba ya Diamond.
“Mwee, huyu ndiye Zari wa Diamond! Hivi mimba anayo kweli au ndiyo haya mambo ya mastaa wetu, mhh lakini kweli kitumbo kama kimetuna vile,” alisikika akisema mmoja wa wanawake hao.Uwepo wa mwanadada huyo uliwafanya wengi kusahau ishu ya msiba na kujikuta wakipigana vikumbo kumshangaa Zari ambaye muda mwingi alikuwa akijificha.
Kutokana na mazingira ya watu kukanyagana kutaka kumuona staa huyo, mrembo aliyefahamika kwa jina la Jestina George aligeuka kuwa bodigadi wake ili kumuepushia usumbufu ambapo alifanya kazi ya kumlinda.
PAPARAZI AZUIWA KUMPIGA PICHA
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la msiba kwa lengo la kupata picha za kumbukumbu kwamba Zari aliwahi kufika eneo hilo, alikumbana na wakati mgumu baada ya Jestina kumpiga mkwara asijaribu kupiga picha.
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la msiba kwa lengo la kupata picha za kumbukumbu kwamba Zari aliwahi kufika eneo hilo, alikumbana na wakati mgumu baada ya Jestina kumpiga mkwara asijaribu kupiga picha.
“Weee, ukijaribu kupiga picha tunakorofishana, mwenyewe hataki kupiga picha, kama vipi nenda kamuombe ruhusa Diamond,” alisema Jestina huku akimficha Zari
Post a Comment
Comment hapa