Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema
kuwa migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel
Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.
Akipiga stori na mnoko wetu, Bozi alisema tatizo kubwa lililomkuta
Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya kupuuza
penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake za utupu
alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano.
“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi
langu akaona anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye
mitandao ya kijamii, jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini
yaliyomtokea ni laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa
kitendo kile cha ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.
Post a Comment
Comment hapa