Wikiendi iliyopita, gumzo kubwa katika
mitandao ya kijamii lilikuwa ni kuhusu stori ya staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufunga ndoa na mwandani wake, Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’ lakini ukweli wake sasa umejulikana.
Taarifa hizo ziliibuka katika mtandao wa
Instagram mara baada ya Diamond kuweka picha iliyomuonesha akiwa na Zari
ambaye alivaa shela huku Diamond akiwa na suti kuashiria kuwa wawili
hao wamefunga ndoa kutokana na ujumbe uliosindikiza picha hiyo.
Diamond aliandika: “Wakati mwingine usiri
una baraka zaidi...alhamdullah (sometimes privacy has more
blessings...thank you so much God).”
Baada ya ujumbe huo ndipo mashabiki wao walipoanza kusambaziana ujumbe kuwa Diamond amemuoa Zari.
Baada ya kuenea kwa ubuyu huo, mnoko
wetu alimvutia waya Diamond na kumtaka aeleze ukweli wa habari hiyo
ambapo alifunguka.
Mnoko: Ebwana vipi hii ishu ya ndoa ni kweli umeoa?
Diamond: Suala la ndoa lipo tu kwani wewe hujui mtoto Zari ana familia yangu? Nikikamilisha mchakato naweka wazi kila kitu.
Mnoko: Kwa hiyo unataka kuwaambia Watanzania kwamba umeshamuoa Zari au bado?
Diamond: Taratibu za awali nyingi
tumeshakamilisha lakini zaidi kuna kitu kikubwa natarajia kukifanya pale
Mlimani City (Dar) na hiki kitathibitisha ukweli wa unachokiuliza.
Mnoko: Umesema nisubiri sawa, hiyo Mlimani City ni tarehe ngapi?
Diamond: Usijali ni Mei Mosi, mwaka huu.
Mnoko: Poa, kila la kheri tutajumuika pamoja siku hiyo.
Mara kadhaa Diamond amekuwa akionesha nia ya kumuoa Zari hivyo mashabiki wengi wanaamini kuwa safari hii yupo ‘siriaz’ zaidi.
Post a Comment
Comment hapa