Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’,
amesema hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo
hazijatoka ambapo asilimia kubwa alishazilipia.
“Sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo
zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia
ambapo kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha
kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye,” alisema Suma
Lee akizungumza na mnoko.
Ameongeza kuwa Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia,
wengine walikuwa hawataki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna
wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.
Post a Comment
Comment hapa